22.7 C
Dar es Salaam
Saturday, July 31, 2021

BREAKING NEWS: CCM YAVUNJA UKIMYA KUHUSU KATIBA MPYA

- Advertisement -spot_imgspot_img
- Advertisement -spot_imgspot_img

Chama Cha Mapinduzi kimesema hakina  agenda ya katiba mpya kwa wakati  huu  badala yake kipaumbele zaidi kimewekwa katika kujenga  nchi kwa ukamilishaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, kupambana na umasikini, kuboresha huduma za kijamii, kuboresha mazingira ya biashara, kuzidisha ustawi wa demokrasia, kusimamia utawala bora, kulinda sambamba na kuheshimu haki za binadamu.
Hivyo  hakiwezi kuacha masuala hayo  ya msingi yaliyobeba mustakabali wa Taifa na kuanza kurudi nyuma kimaendeleo kwa maslahi  binafsi ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ameyasema hayo wakati akizungumza na wazee mbalimbali wa wilaya ya Tanga mjini katika ukumbi wa halmashauri ya Jiji la Tanga.
Amefahamisha kuwa serikali ya ya Rais Samia inakimbizana na vipaumbele vya msingi zaidi katika maeneo mtambuka ya upatikanaji wa  huduma bora  za afya, utoaji  wa elimu bure na bora mashuleni na vyuoni,  huduma za maji safi na salama zikiimarishwa katika maeneo hasa yasiyo na huduma hiyo,  kuimarishwa kwa mfumo wa utoaji haki, kutoa  mikopo ya riba ndogo na masharti nafuu, kuboresha  kilimo na kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya mazao  sambamba na kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wafanyabishara na wawekezaji huku mkazo zaidi ukielekezwa katika  kukomesha  rushwa na ubadhirifu jambo ambalo litasaidia katika  matumizi yenye tija ya utajiri wa nchi kupitia rasilimali zake.
“Hakuna mwananchi anayesema serikali iyaache yote hayo ishughulike kwanza na katiba mpya hayupo. Madai ya katiba mpya sio agenda ya kisiasa hivyo wanasiasa waache kuitumia agenda hiyo kama turufu ya kuwahadaa wananchi kuwa hilo ndio jawabu la changamoto zao jambo ambalo sio kweli” alisema Shaka
Shaka alibainisha kuwa Taifa linahitaji viongozi waadilifu, wazalendo, wanaothamini utaifa wetu, wanaotanguliza na kuweka mbele maslahi ya Taifa ili kuwanufaisha wananchi sio wanasiasa mahiri wa propaganda za kutafuta ushawishi wa kutafuta kuungwa mkono kisiasa bila kujenga misingi madhubuti ya taasisi zao za kisiasa zinazotumika kubeba agenda hizi za wananchi.
“Watu wasipotoshe,  Mchakato wa kutungwa kwa Katiba mpya uliendeshwa na ulifikia hatua ya Katiba inayopendekezwa iliyopitishwa na Bunge Maalumu la Katiba ambayo inasubiri kupigiwa kura ya maoni na wananchi pale ambapo serikali itaona inafaa kukamilisha mchakato wake hivyo upinzani uache hadithi za kusadikika. Huu ni wakati wa kujenga nchi kwanza kazi ambayo CCM inaifanya baada kuaminiwa na watanzania” Alibainisha Shaka
Hata hivyo katibu huyo wa itikadi na Uenezi Ndugu Shaka amekumbushia kuwa hata vyama vya MCP,  KANU na UNIP viliondolewa madarakani kwa katiba ile ile na baadae MCT cha Malawi kikarudi tena madarakani kwa katiba ileile kutokana na  uamuzi  wa wapiga kura  wala sio kwa  katiba mpya au ya zamani kwani  kinachoweka chama  madarakani ni sera bora, utekelezaji madhubuti, na uwezo wa kuwaunganisha wananchi katika kuwaletea maendeleo endelevu kwa usawa kama ifanyavyo CCM. 
“Hata ukiangalia hoja ya  suala la tume huru  ya uchanguzi nalo ni jambo la kikatiba ndio  maana CCM inaendelea kushangaa upinzani wanavyozungumzia katiba mpya na tume huru ya uchaguzi  kama ajenda mbili tofauti  utadhani katiba ni jambo jingine na tume ni jambo jingine. Tume  ya uchaguzi ipo kikatiba na haijawahi kubadilishwa, ni tume hiyo hiyo iliyowapa madiwani, wawakilishi na wabunge kwa zaidi ya miaka 20 tena hata wakati mwingine wakiongezeka kwa idadi ajabu tume hiyo hiyo wanataka iwe huru, sasa sijui ni uhuru upi wanautaka labda wanataka waiongoze wao japo bado watashindwa chaguzi maana hawataki kukubali wana vyama vya siasa dhaifu!” alisema Shaka.

All right. Well, take care yourself. I guess that’s what you’re best, presence old master? A tremor in the Force. The last time felt it was in the presence of my old master. I have traced the Rebel spies to her. Now she is my only link to finding their secret base. A tremor in the Force. The last time I felt it was in the presence of my old master.

- Advertisement -spot_imgspot_img
Latest news
- Advertisement -spot_img
Related news
- Advertisement -spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here