22.7 C
Dar es Salaam
Saturday, July 31, 2021

Azam FC yaachana na Kahata

- Advertisement -spot_imgspot_img
- Advertisement -spot_imgspot_img

KUNA tetesi kuwa Uongozi wa Azam FC rasmi wametangaza kuachana na mipango ya kumsajili aliyekuwa kiungo mchezeshaji fundi raia wa Kenya, Francis Kahata.

Awali, Azam na Yanga walitajwa kuingia kwenye vita ya kuwania saini ya kiungo huyo rasta ambaye hivi sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika wiki iliyopita kabla ya kurejea kwao Kenya.

Taarifa ni kwamba uongozi wa timu hiyo umejiridhisha kuwa kiungo huyo hatasajiliwa huku wakiweka mipango mingine katika usajili wa msimu ujao.

Chanzo maalum kilisema kuwa uongozi wa timu hiyo una mikakati mizito ya kutengeneza kikosi imara kitakachofanya vizuri katika michuano ya kimataifa, mwakani.

Ilielezwa kuwa tayari wana orodha ya wachezaji waliopo katika mipango yao lakini siyo Kahata ambaye hakuwa anapata nafasi ya kucheza katika kikosi cha Simba.

“Kahata aliwahi kuletwa kwa uongozi kwa ajili ya kukamiliksha mipango ya kumsajili, lakini ikashindikana kutokana na mipango yetu tuliyokuwa nayo katika kukisuka kikosi kitakachokuwa imara na tishio.

“Hivyo Kahata rasmi tumesitisha mipango yetu ya kumsajili na badala yake tumemuacha aende kwingine, atakapotaka kwenda kucheza lakini siyo Azam,” Kilisema chanzo hicho.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Muda wetu wa usajili bado na kila kitu kitajulikana mara baada ya ligi kumalizika.

- Advertisement -spot_imgspot_img
Latest news
- Advertisement -spot_img
Related news
- Advertisement -spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here