24.1 C
Dar es Salaam
Saturday, July 31, 2021

MAWAKILI JINOENI: AG-KILANGI

- Advertisement -spot_imgspot_img
- Advertisement -spot_imgspot_img

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi,amewataka Mawakili wa Serikali nchini kuendelea kujielimisha kila siku kutokana na kukua kwa taaluma ya Sheria ili kuongeza ufanisi kwenye utekelezaji wa majukumu yao

 Wito huo ameutoa jana jijini Dodoma wakati  akifungua mafunzo ya siku nne yenye lengo la kuwajengea uwezo Mawakili wa serikali kwenye uendeshaji wa mashauri yanayofunguliwa dhidi ya serikali yaliyoandaliwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Prof.Kilangi alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu na yatasaidia kuwanoa Mawakili hao ili kuendana na mabadiliko ya taaluma ya Sheria ambayo yamekuwa yanatokea kila siku ulimwenguni.

“Mafunzo haya ni kwa ajili ya kuwaongezea ujuzi na weledi katika utekelezaji wa majukumu yenu na kuboresha mahusiano jambo ambalo ni muhimu katika utendaji kazi, mada muhimu zitagusiwa ikiwamo weledi katika uendeshaji wa mashauri ya madai,”alisema Prof.Kilangi

Prof.Kilangi alisisitiza kuwa mada hizo ni muhimu kwao katika uendeshaji wa mashauri ya serikali ndani na nje ya nchi.

“Lazima muwe na ujuzi wa kusimamia na kuendesha mashauri haya ndani na nje ya nchi inaweza kuwa kwenye Mahakama za Kimataifa au Mabaraza ya kimataifa,”alisema Prof.Kilangi

Pia aliitaka  Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kushirikiana na Taasisi mbalimbali katika kutatua changamoto  mbalimbali zinazoikabili  ofisi hiyo  ikiwemo uhaba wa mawakili wa Serikali.

Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata ,alisema ofisi hiyo ilipewa jukumu lakuendesha madai ya kesi ndani na nje ya nchi na kupitia mafunzo hayo yanaenda kuwaweka katika mtazamo mmoja wa uendeshaji wa mashauri kwa niaba ya Serikali na Taasisi zake huku akibainisha mafanikio na changamoto mbalimbali.Wakili Malata alisema kuwa ndani ya miaka mitatu Ofisi yke imeokoa zaidi ya Sh.Trilioni 12 katika mashauri ya madai yaliyokuwa yamefunguliwa dhidi ya serikali.

Alisema kuwa  ofisi hiyo ilianza kutekeleza majukumu yake mwaka 2018 na kwa kipindi hicho mafanikio mbalimbali yamepatikana ambapo kwa mwaka wa fedha 2019/20 ofisi hiyo ilifanikiwa kuokoa fedha ambazo zinatokana na mashauri yaliyofunguliwa dhidi ya serikali na taasisi zake Sh.Trilioni 11.4

“Mwaka huo pia ofisi iliendesha mashauri mbalimbali ambayo hayahusishi fedha na kurejesha mali mbalimbali ikiwamo mashamba 106,”alisema Malata.Hata hivyo Malata alielezea  changamoto zinazowakabili ni uhaba wa mawakili ambapo walipo ni 88 huku mahitaji ni Mawakili 308 pamoja na uhaba wa usafiri.Mwishoo

- Advertisement -spot_imgspot_img
Latest news
- Advertisement -spot_img
Related news
- Advertisement -spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here