24.1 C
Dar es Salaam
Saturday, July 31, 2021

Taifa Stars, yawatoa jasho Malawi kwa Mkapa

- Advertisement -spot_imgspot_img
- Advertisement -spot_imgspot_img

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars jana walikuwa na kibarua kizito mbele ya Wamalawi katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. 

Ikumbukwe mchezo huo, ulikua wa kirafiki kwa mujibu wa Kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Mechi hiyo, iliaza kwa kasi huku kila upande ukijaribu kupata goli la kuongoza mapema hata hivyo milango ilikuwa migumu.

Malawi, walionekana kuliandama kwa kipindi kirefu lango la Stars na kusababisha kona za mara kwa mara ambazo hata hivyo hazikuzaa matunda.

Aidha, Stars ndio walikua wa kwanza kulikaribia lango la Wamalawi kunako dakika ya pili ambapo Bocco alifanya jaribio ambalo lilikwenda nje ya lango. 

Dakika ya 10 Malawi wanapeleka mashambulizi mlangoni kwa Taifa Satar na kuokolewa.

Dakika ya 17 Malawi wanapata kona inapigwa na Banda lakini iliokolewa na kuwa kona nyingine ambayo haikuzaa matunda.

Hadi timu hizo zinakwenda mapunzi kulikuwa hakuna mbabe.

Kipindi cha pili timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu ambapo hadi gazeti hili linakwenda mitamboni kunako dakika 75, Taifa Stars walikuwaa mbele kwa bao 2-0

Mabao hayo yaliwekwa kimiani na na John Bocco akimalizia pasi ya Kibu Denis huku lile la pili likifungwa na Mwenda.

- Advertisement -spot_imgspot_img
Latest news
- Advertisement -spot_img
Related news
- Advertisement -spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here